Mamlaka ya Usafiri wa Majini na nchi kavu Tanzania (SUMATRA) imesema ipo kwenye maandalizi na mjadala kuhusiana na mabasi yanayofanya safari zake mikoani kuruhu  safari zake kufanyika kwa masaa 24 na kusema kwa kufanya hivyo itasaidia kupunguza msongamano wa mabasi barabarani.

Mkurugenzi wa Sumatra, Gilliard Ngewe amesema wananchi wanauhitaji mkubwa kufanya safari zake uskiu na mchana.

“Tupo kwenye maandalizi bado hatujaamua mambo yakikaa sawa tutakwenda na utaratibu huo wa saa 24’’. amesema Ngewe.

Ambapo amesema watu wangependa wafanye kazi muda wote na matumizi ya magari yenyewe yanaweza yakaenda na yakarudi, lakini pia kupunguza msongamano wa mabasi pale Ubungo  kulinganisha na hali ya sasa.

Aidha amesema ikiwa mabasi yatafanya kazi kwa masaa 24 yatapeana nafasi, na mwisho wa mwaka mabasi baada ya kwenda kulala mahali, yanaendelea na safari zake.

Hivi karibuni mamlaka hiyo ilikuwa hairuhusu mabasi kufanya safari zake nyakati za usiku kwa kuhofia usalama na ajali za barabarani, wakisema kwamba madereva huwa wanajisahau wanapokuwa barabarani hasa nyakati za usiku.

Luoga aanza kazi rasmi na mikakati mizito
JPM awabadilikia Mawaziri