Kocha  wa Yanga, Mwinyi Zahera ametenga kitita cha milioni mbili kwa ajili ya kununua mabao atakayo funga mshambuliaj wake David Molinga ‘Falcao’ raia wa DR Congo katika Ligi Kuu Bara.

Zahera amesema  kwamba atatoa kiasi hicho cha milioni 2,293,230 sawa na dola 1,000  endapo kama itatokea straika wake  huyo atashindwa kufunga mabao 15  au zaidi kwenye ligi kuu.

“Mimi ninasema nitatoa kiasi cha  dola 1,000 kama itatokea Molinga  hatafunga mabao 15 kwenye ligi kuu ninamjua ana uwezo mkubwa wa  kufunga tofauti na watu ambavyo  wanamchukulia,” alisema Zahera.

“Hapa kwenye kikosi changu tatizo  lililopo ni washambuliaji tu kushindwa  kufunga mabao. Sisi kwenye mechi  moja tunaweza kupata hadi nafasi sita  lakini tukafunga mabao machache  huku nyingi tukikosa.

“Yaani hatuna shida kabisa kwenye  kutengeneza pasi za mabao ila tatizo  ni kufunga lakini muda si mrefu  nitatengeneza mbinu ambayo itafanya  tufunge katika kila nafasi ambayo  tunaipata,” alisema Zahera.

Kocha huyo ametenga kitita hiko ikiwa  ni baada ya mshambuliaji wake huyo kuanza  kuonyesha cheche kwa kufunga  mabao matatu kwenye mechi zao  mbili zilizopita za kirafiki.

Molinga alifunga  mabao hayo  kwenye mechi za  timu hiyo dhidi  ya Pamba SC  na Toto  African  wakati  walipokuwa  Mwanza  wiki chache  zilizopita.

Askofu mkuu Dar es salaam, Ruwa’ichi atolewa ICU
Rais Magufuli: aliyeshikilia ndege Afrika Kusini 'ni wivu tu'