Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini Kongo wamesema kuwa wana wasiwasi mkubwa kutokana na kuendelea kwa mauaji ya raia katika jimbo la Ituri na Kivu ya kaskazini licha ya kuwepo kwa jeshi na vikosi vya umoja wa mataifa.

Katika taarifa yao ya pamoja maaskofu wa Kongo wamesikitishwa pia na kutokuweko kwa mabadiliko ya hali ya kiuchumi na kijamii miezi kadhaa baada ya kuapishwa kwa rais mpya nchini humo’ Felix Tshisekedi.

Aidha, kwenye ujumbe wao uliopewa kichwa cha habari ‘Komboeni Umma Wangu’ kutokana na maandishi ya bibilia, maskofu wa Kongo wameeleza kwamba kwa ujumla hali ya kiusalama, kisiasa ,kiuchumi na kijamii nchini humo bado haijawaridhisha waliowengi.

Maaskofu hao wamesema kuwa hawaoni kwa nini jeshi linaloungwa mkono na vikosi vya umoja wa mataifa vya MONUSCO vimeshindwa kutokomeza makundi ya wapiganaji ya kitaifa na yale ya kimataifa yakiwemo ADF, LRA na FDLR na wavamizi wa Mbororo ambao wote wanasumbua na kuua raia wasionahatia ,huku kukiwa na hisia ya kutokuweko mamlaka ya serikali.

DataVision International yashinda tuzo ya ‘Brand Leadership’ Afrika Mashariki
Video: Mazingaombwe ya AJABU zaidi Duniani | Hawa Wamefariki dunia wakionyesha Mazingaombwe yao LIVE

Comments

comments