Maandalizi ya tamasha la vyakula vya asili linalotarajiwa kufanyika Zanzibar kwa mara ya tatu yameshakamilika, ambapo tamasha hilo pia linatarajiwa kuimarisha sekta ya utalii nchini.

Mtaalam wa masuala ya chakula na utamaduni Zanzibar, Farid Hamid amethibitisha kukamilika kwa maandalizi hayo na kusisitiza kuwa tamasha hilo litaanza oktoba 14, mwaka huu siku ya jumapili ambapo zaidi ya migahawa 20 inatarajiwa kushiriki katika tamasha hilo.

Maonyesho hayo yatadumu kwa siku saba na kutakuwa na vyakula asili kutoka mataifa mbalimbali ikiwemo Zanzibar. ambapo tamasha hilo litavutia watalii wengi kwakuwa eneo litakalo tumiwa kuonyesha ni forodhani ambapo ni miongoni mwa eneo pendwa kwa watalii.

Aidha, tamasha hilo linatarajiwa kubadili mtazamo wa visiwa hivyo ambao bado upo nyuma katika matumizi ya vyakula asili hivyo tamasha hilo litasaidia kuongeza ushawishi kwa wahudumu wa migahawa kuvipa kipaumbele vyakula vya asili katika utoaji wa huduma zao.

Video: Kangi Lugola afunguka makubwa kuhusu 'Mo Dewji'
Akiri kuua wanawake sita kwa imani za kishirikina