Chama cha ACT – Wazalendo kimemchagua Maalim Seif kuwa Mwenyekiti wao mpya usiku wa tarehe 14 Machi 2020, huku Zitto kabwe akichaguliwa kwa mara ya pili kuwa kiongozi wao mkuu.

Maalim Seif ambaye anakuwa mwenyekiti wa pili tangu kuanzishwa kwa chama hicho 2014, ameshinda kwa kura 337 huku mpinzani wake wa pili akipata kura 20 na mwingine akipata kura 4.

Katika Uchaguzi huo uliofanyika usiku wa kuamkia leo,  Zitto Kabwe kachaguliwa kuendelea na nafasi yake ya Kiongozi Mkuu wa chama kwa kura 276 sawa na asilimia 73.6, huku mshindani wake Ismail Jussa akipata kura 92 sawa na asilimia 24.2, ambapo kura nane zimekataliwa.

Akitangaza matokeo hayo, mwenyekiti wa kamati maalumu ya uchaguzi wa chama hicho, Omar Said amesema jumla ya wajumbe walioshiriki mkutano huo ni 375, kura halili zilikuwa 367 na zilizoharibika 8.

Uchaguzi huo unaendelea leo katika nafasi mbalimbali ikiwemo ya makamu mwenyekiti Zanznibar, na bara kisha kesho nafasi ya katibu mkuu.

 

Wamnyonga mtoto wa miezi 9 ili waoane
Video: Wabunge 50 wa CCM walivyoitosa Chadema, Waliokimbizwa hospitali Moshi hawana corona

Comments

comments