Kamati Kuu ya Chama cha ACT-Wazalendo iliyoketi Juni 9 na 10, imefanya uteuzi wa viongozi wa kitaifa ili kuboresha safu ya uongozi wa kitaifa wa chama hicho.

Miongoni mwa viongozi walioteuliwa ni pamoja na Maalim Seif Hamad ambaye sasa ameteuliwa kuwa Mshauri Mkuu wa Chama, ikiwa ni moja ya ngazi kubwa katika chama hicho.

Aidha, viongozi wengine walioteuliwa katika mkutano huo ni, nafasi ya wajumbe wanne wa Kamati Kuu ya chama ambao ni, Theopista Kumwenda, Mwajabu Dhahabu, Fatma Fereji, Eddy Riyami. Wengine ni Wenyeviti na Makatibu wa Kamati za Kitaifa.

Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha na Miradi ni Nassor A. Marzurui, Mwenyekiti wa Kamati ya Itikadi, Mawasiliano na Uenezi ni Salim A. Bimani, Mwenyekiti wa Kamati ya Kampeni na Uchaguzi, Joram Bashange, Mwenyekiti wa Kamati ya Oganaizesheni, Mafunzo na Wanachama, Mhonga Ruhwanya na Mwenyekiti wa Kamati ya Mikakati, Usimamizi na Ufuatiliaji, Ismail Jussa.

Ikumbukwe kwamba Maalim Seif pamoja na wafuasi wake walihamia ACT- Wazalendo kutokea Chama cha Wananchi CUF kufuatia mgogoro wa muda mrefu ndani ya chama hicho.

LIVE IKULU: Rais Magufuli akiwaapisha viongozi na kupokea Gawio kutoka kampuni ya BHATI AIRTEL
Video: Mawaziri 7 ambao hawajaguswa na JPM, Utata wagubika kifo kigogo wa polisi