Maafisa wa huduma za dharura Indonesia wameonya kuongezeka kiwango cha hatari ya mlipuko wa Volcano katika mlima wa Anak Krakatau.

Mlipuko huo mapema wiki iliyopita ulipelekea mawimbi makubwa ya uharibifu kutokana na Tsunami kupiga katika pwani ya magharibi ya nchi hiyo ambayo ilisababisha vifo vya watu wapatao 430.

Maafisa wa dharura wameweka onyo la watu kutokaribia eneo la mlima huo wa Anak Krakatau ambao unaonekana utaripuka tena wakati wowote.

Aidha, vyanzo vya habari vimesema onyo la pili linalotahadharisha mlipuko huo wakati mlima huo ukiendelea kutoa gesi ya moto na volcano nyingine kwenye bahari pamoja na wingu zito la majivu angani.

Maafisa wameongeza kuwa eneo la kuzunguka volcano limefikia kilometa 5 wakati harakati za milipuko zikiendelea na mawimbi makubwa ikiashiria kwamba mawimbi mengine makubwa zaidi ya uharibifu yanaweza kupiga.

Hata hivyo, Maafisa wa mamlaka ya usafiri wa anga wameonya ndege zisiruke kuelekea katika eneo hilo.

 

Video: JPM arejesha furaha kwa wafanyakazi,'Haiwezekani waendelee kunyonywa'
Raia wa Ufaransa aanza safari ya kuvuka bahari kwa Pipa

Comments

comments