Serikali imebaini wananchi 231 wanadaiwa kodi ya pango la ardhi kiasi cha shilingi milioni 271 katika Manispaa ya Musoma Mjini Mkoani Mara.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi baada ya kufanya ukaguzi wa mfumo wa kodi ya ardhi.

Aidha, Lukuvi ametaka majina ya wadaiwa hao yawasilishwe mahakamani ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kupiga mnada majengo na mali zao kama wakikaidi kulipa kodi hiyo.

“Nimeagiza kesi za madai ya kodi zitolewe hukumu ndani ya siku moja tu ili wadaiwa waweze kuchukuliwa hatua ya kuuzwa kwa mali zao haraka,”Amesema Lukuvi.

Katika hatua nyingine, Lukuvi amefanya uzinduzi wa mpango kabambe (Master Plan) wa Manispaa ya Musoma na kuwapongeza viongozi na watendaji wa Manispaa ya Musoma kwa kuwa Manispaa ya kwanza nchini kuweza kuzindua mpango kabambe wa mji wao.

Hata hivyo, Lukuvi amewataka Viongozi wa Manispaa zote nchini kusimamia suala la ujenzi unaofuata mipango miji na kupiga marufuku wananchi wanaojenga bila kupewa vibali vya ujenzi katika maeneo ambayo yamekamilisha mipango kabambe na kuagiza nyumba itakayojengwa bila kibali ivunjwe.

Pia amewataka maafisa ardhi wa manispaa kutoa elimu ya masuala ya Ardhi kwa kwa maafisa watendaji wa Mitaa ili elimu na utekelezaji wa masuala ya ardhi ngazi ya wananchi uwe ni kwa urahisi na wenye kueleweka

Video: Maalim Seif, Prof. Lipumba ni msuli msuli, Arobaini za vyeti feki leo
Magazeti ya Tanzania leo Aprili 28, 2017