Wakati kombe la dunia likielekea kileleni wiki hii, harakati za panga pangua kwenye vilabu vya soka nazo zinazidi kupamba moto. Kwa msemo wa mtaani uliovuma, ‘mambo ni hiviii…’.

Mshambuliaji wa zamani wa Manchester United, Luís Carlos Almeida da Cunha, maarufuku kama ‘Nani’ amerejea rasmi kwenye klabu iliyomkuza ya Sporting CP .

Mshambuliaji huyo alithibitishwa rasmi kurejea klabuni hapo usiku wa kuamkia leo, baada ya uongozi wa klabu ya Sporting CP kukamilisha mpango wa kumsajili akitokea Valencia ya Uhispania.

Msimu uliopita, Nani aliitumikia klabu ya SS Lazio ya nchini Italia kwa mkataba wa mkopo akitokea Valencia CF.

Akiwa klabuni hapo akiutumikia mkataba wake wa mkopo msimu wa 2014/15, Nani alicheza michezo 36 na kufanikiwa kufunga mabao 11.

Uongozi wa Valencia umethibitisha kuondoka kwa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 31, kama mchezaji huru, kufuatia makubaliano maalum ambayo yameonesha wazi kutoa nafasi kwa mchezaji huyo kurejea nyumbani.

Nani ambaye alikua sehemu ya kikosi cha timu ya taifa ya Ureno kilichotwaa ubingwa wa Ulaya mwaka 2016, amekuwa na wakati mgumu wa kuonesha uwezo wake kisoka na kushindwa kudumu kwa zaidi ya msimu mmoja kwenye klabu inayomsajili.

Baada ya kuondoka Man Utd mwaka 2015, mshambuliaji huyo alitimkia Fenerbahce ya Uturuki (2015–2016), Valencia (2016-2018) lakini kwa msimu wa 2017-2018 alipelekwa kwa mkopo SS Lazio.

Lugola alivyotofautiana na Mzee wa Upako
Video: COSTECH yatoa ufafanuzi kuhusu barua iliyosambaa juu ya Twaweza