Mshambuliaji wa zamani wa Man Utd Luís Carlos Almeida da Cunha *Nani* amerejea kwenye klabu iliyomkuza Sporting CP .

Mshambuliaji huyo alithibitishwa rasmi kurejea klabuni hapo usiku wa kuamkia leo, baada ya uongozi wa klabu ya Sporting CP kukamilisha mpango wa kumsajili akitokea Valencia ya Hispania.

Msimu uliopita Nani aliitumikia klabu ya SS Lazio ya nchini Italia kwa mkataba wa mkopo akitokea Valencia CF.

Akiwa klabuni hapo kwa mkopo msimu wa 2014-15, Nani alicheza michezo 36 na kufunga mabao 11.

Kwa upande wa uongozi wa klabu ya Valencia umethibitisha kuondoka kwa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 31, kama mchezaji huru, kufuatia makubaliano maalum ambayo dhahir yameonyesha kutoa nafasi kwa Nani kurejea nyumbani.

Nani ambaye alikua sehemu ya kikosi cha timu ya taifa ya Ureno kilichotwaa ubingwa wa Ulaya mwaka 2016, amekua na wakati mgumu wa kuonyesha uwezo wake kisoka na kushindwa kudumu kwa zaidi ya msimu mmoja kwenye klabu inayomsajili.

Baada ya kuondoka Man Utd mwaka 2015, mshambuliaji huyo alitimkia Fenerbahce ya Uturuki (2015–2016), Valencia (2016-2018) lakini kwa msimu wa 2017-2018 alipelekwa kwa mkopo SS Lazio.

COSTECH yatoa ufafanuzi kuhusu barua iliyosambaa juu ya Twaweza

Comments

comments