Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugola ameagiza kuchukuliwa hatua za kisheria kwa wanasiasa ambao wanafanya mikutano ya ndani ambayo imepigwa marufuku.

Ametoa kauli hiyo akiwa Mkoani Morogoro wakati akizungumza na wananchi wa Mjini Kilosa ambapo amesema ana taarifa za kuwepo kwa baadhi ya wanasiasa wa upinzani wanaofanya vikao vyao vya ndani huku wakitoa kauli ambazo zinaashiria uchochezi.

“Mimi Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, sitakubaliana na kiongozi wa chama chochote kuvunja agizo tulilolitoa nchi nzima kwa kutoruhusu kufanyika mikutano ya hadhara ya siasa, na pia kupitia mikutano ya ndani ambayo inafanyika, baadhi ya wanasiasa wahuni wanamtukana Rais ambaye ndiyo kiongozi Mkuu wa nchi, mimi sitakubaliana na hilo,” amesema Lugola.

Aidha Lugola amesema Rais Magufuli ni kiongozi ambaye kwa muda mfupi ameiletea mabadiliko makubwa nchi na pia ana mipango mikubwa ya maendeleo yanayokuja katika uongozi wake.

Makala: Lowassa ataishi vipi na CCM hii? Sababu halisi za kurudi hizi hapa
Video: Lowassa kutikisa uchaguzi CCM, Hatma ya waliomteka Mo wiki hii.