Kocha Mkuu Young Africans Luc Eymael amekiri kikosi chake kilikua na udhaifu mkubwa mbele ya Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC, wakati wa mchezo wa Nusu Fainali Kombe La Shirikisho (ASFC) Jumapili.

Katika mchezo huo Young Africans walikubali kichapo cha maabo manne kwa moja, na kutupwa nje ya michuano ya ASFC sambamba na kupoteza nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa msimu ujao 2020/21.

Kocha Eymael amesema kila aliyeufuatilia mchezo huo aliuona upungufu yaliyokuwa chanzo cha kupoteza kwa idadi kubwa ya mabao. Hivyo ameahidi kushughulikia mapungufu hayo ili kuwa na kikosi imara msimu ujao.

“Ubora wa wachezaji wangu katika mchezo dhidi ya Simba haukuwa mzuri kama ambavyo tulivyodhani kabla. Natakiwa kukutana na viongozi kujadili usajili wachezaji wenye uwezo kuanzia wazawa hadi wakigeni, na hili ndio jambo la msingi,”

“Mchezo ule umetupa mwongozo katika usajili, tusajili wachezaji kweli na wenye sifa ya kuichezea Yanga na wakaja kuipigania katika mashindano pamoja na michezo migumu kama ile ya watani.

“Jambo jingine ni kufanya mabadiliko ya dhati, tunatakiwa kubaki na wachezaji wenye sifa za kuichezea Yanga na si vinginevyo.” Amesema kocha huyo kutoka Ubelgiji.

Makonda ajitosa Kigamboni, Msukuma, Kanyasu warudi Geita
Mnyika hagombei Ubunge, kujenga chama kama Nyerere