Kocha Mkuu wa Young Africans, Luc Eymael amesema haelewi kwa nini  viongozi wa klabu hiyo mpaka sasa wameshindwa kukamilisha utaratibu wa kumwezesha kurejea Tanzania kwa ajili ya kuendelea na kazi ya kinoa kikosi chake.

Kikosi cha Young Africans kilianza kujiandaa na michezo ya ligi kuu Tanzania Bara (VPL) na Kombe la Shirikisho (ASFC), juma lililopita chini ya kocha msaidizi Charles Boniface Mkwasa.

Aymeal ambaye yupo Ubelgiji amesema, zimebaki siku 10 tu kuanza kwa michezo ya ligi kuu Tanzania Bara, Ila hujui ni lini atarejea Tanzania.

Kocha huyo ameushangaa Uongozi wa Klabu hiyo kwa kushindwa kufanya taratibu mapema kwa kusema Azam wameweza kuwarejesha makocha wao nchini lakini kwake hajui kwa nini imeshindikana mpaka Sasa.

“Viongozi wa Yanga wananiambia wameshindwa kunikatia tiketi ya ndege kwenye system, kama wameshindwa kunikatia katika system basi wangenikatia online”

“Ni vizuri kusaini mkataba na La Liga lakini kama unataka kuwa club kubwa kwanza jaribu kumrudisha kocha wako haraka iwezekanavyo kama una muheshimu”

Vyuo vyapewa siku 3 kukamilisha mgao fedha za kujikimu kwa wanafunzi
Mahakama yatupilia mbali kesi dhidi ya Ndugai kutambua ubunge wa Mwambe