Waziri Mkuu aliyejiuzuru na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Edward Lowassa amewataka wanachama na viongozi wa Chama hicho kuacha kumtaja taja mgombea Ubunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Kinondoni, Maulid Mtulia kwani mtu huyo ni wa hovyo hastaili kutajwa tajwa kwani kufanya hivyo ni kumpa umaarufu.

Ameyasema hayo katika uzinduzi wa kampeni za uchaguzi wa marudio jimbo la Kinondoni ambapo amemnadi mgombea wa chama hicho, Salum Mwalimu kuwa ndiye anafaa kuliongoza jimbo hilo.

“Kwanza nawashauri huyu Mtulia msimseme seme sana wanini huyu, mtu hovyo kabisa huyu mnampa kichwa tu sasa mtu hovyo hapaswi kuchukua muda wenu kumjadili bali nachotaka tushughulike kuwaelimisha wananchi wa Kinondoni kwanini wanastahili kutupa sisi kura, habari ya huyu bwana tuachane naye, hawa CCM wa hovyo kweli, hawaeleweki kule Moshi na Korogwe tulishinda lakini wakaja kusema tumeshindwa hivyo nataka kusema saizi tujiandae kulinda kura zetu,”amesema Lowassa

Hata hivyo, Lowassa amesema kuwa mgombea wa chama cha demokrasia na maendeleo ni kijana safi ambaye anastahili kwenda Bungeni kuwasemea wananchi wa Kinondoni.

Gari la wagonjwa latumika kufanya shambulio
Wasira amtaja mchawi wa CCM