Mgombea urais kwa tiketi ya Chadema chini ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Edward Lowassa ametupa karata yake ya kwanza ya ahadi zake kwa watanzania kwa kuwavuta waendesha pikipiki maarufu kama boda boda na mama Lishe maarufu kama Mama Ntilie.

Akiwahutubia maelfu yananchi waliojitokeza kumsindikiza kuchukua fomu ya urais jana jijini Dar es Salaam, Lowassa alisema kuwa endapo atafanikiwa kuingia Ikulu kwa ridhaa ya watanzania, atahakikisha anabadilisha hali ya maisha ya watanzania kiuchumi na kwamba ataunda serikali itakayokuwa rafiki kwa Boda Boda na Mama Ntilie ili kuhakikisha wanainuka zaidi kiuchumi.

“Muweke matumaini yenu pale, mimi nawahakikisheni kazi yangu ya kwanza Mungu akibariki nikaingia Ikulu nitaanza na vijana. Nachukua dhamana ya kushughulika na matatizo ya vijana. Na nitaunda serikali ambayo itakuwa rarafiki wa Mama Ntilie, rafiki wa Machina na rafiki wa Boda Boda.

“Itakuwa priority yangu number one kuangalia watu wangu ambao hali yao ni mbaya. Nawaahidi, kwa jinsi mlivyoniunga mkono, sitawangusha,” aliongeza.

Lowassa alisisitiza kuwa kipaumbele chake cha kwanza ni kuhakikisha anawatoa watanzania katika umasikini waliokuwa nao kwa zaidi ya miaka 50.

MMGL1282

Aidha, Lowassa alieleza kuwa serikali ya Kikwete imeanguka katika suala la maendeleo ya kiuchumi kwa kushuka kwa sarafu na mfumuko wa bei unaowatesa watanzania wa hali ya chini.

Alisisistiza kuwa anauchukia umasikini kama ukoma na kwamba endapo atapewa ridhaa ya kuiongoza serikali ya awamu ya tano atahakikisha anapambana kwa nguvu zote kuuondoa.

Picha kwa hisani ya Michuzi.

‘If You’re Reading This It’s Too Late’ ya Drake Yafika Platinum
Magufuli: Kama Nitakuwa Rais …