Polisi Mkoani Kilimanjaro wamezuia msafara wa waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa kuelekea katika mazishi ya mwanasiasa mkogwe, Peter Kisumo yaliyofanyika jana mkoani humo.

Duru zinaeleza kuwa msafara mrefu wa Edward Lowassa ulizuiwa na polisi katika eneo Mwanga kwa madai kuwa idadi kubwa ya magari na wananchi waliokuwa wakiambatana nae ungehitilafiana na utaratibu wa msiba.

Mzozo wa nusu saa kati ya jeshi la polisi na Edward Lowassa kumtaka apunguze idadi ya magari yaliyokuwa yakiambana naye haukuzaa matunda baada ya mwanasiasa huyo kudai kuwa hawezi kuwaacha watu alioambatana nao kuelekea msibani.

1

Msimamo wa Edward Lowassa ulipelekea kushindwa kuelewana na polisi hivyo kulazimika kuahirisha safari yake ya kuelekea msibani.

Akiongea umati wa wananchi wa eneo hilo waliojitokeza kumlaki wakitaka kuelekea nae msibani, Edward Lowassa aliwataka watulie na kutunza nguvu wanazozitumia siku hiyo kwani atarudi tena eneo hilo kwa ajili yao.

“Asanteni sana kwa mapokezi yenu. Lakini wekeni hizo nguvu pembeni, nitakuja rasmi kwenu. Siku nitakapokuja rasmi nitakuja tena tunakwenda kwenye msiba na sio vizuri kuzungumzia mambo mengine watafikiri tumeleta mambo ya siasa,” alisema Lowassa.

4

Jeshi la polisi mkoani humo limeeleza kuwa lilizuia msafara huo kutokana na kuwepo viashiria vingi vya kisiasa ikiwa ni pamoja na baadhi ya wananchi waliotaka kumsindikiza, kuonekana wakiwa na bendera za vyama vya siasa.

2

Marehemu Peter Kisumo alipumzishwa katika nyumba yake ya kudumu jana, ambapo rais wa Jamhuri ya Tanzania, Dk. Jakaya Kikwete na viongozi wa ngazi za juu wa chama na serikali walihudhuria na kutoa heshima zao za mwisho.

ITV na Radio One wapewa Onyo
Kumbe Mourinho Alimtusi Eva Carneiro (Video)