Aliyekuwa waziri mkuu wa zamani na mjumbe wa kamati kuu ya Chadema, Edward Lowasa amepokelewa rasmi kurudi katika chama cha mapinduzi (CCM) na katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Humphrey Polepole

Akizungumza mara baada ya kukaribishwa rasmi, Lowassa amewashukuru Watanzania milioni 6 waliompigia kura mwaka 2015 na kuwaomba kura hizo wampe rais Magufuli

Amesema kuwa ameamua kurudi CCM kwa kuvutiwa na kazi anazozifanya rais Dkt. Magufuli hivyo amewasihi wananchi wa Monduli kumuunga mkono kwa kazi anazozifanya kwa maendeleo ya Taifa la Tanzania

”Nimerudi nyumbani, sina maneno mengi ila nasema nimerudi nyumbani, Chadema nawashukuru sana neno langu kuu nasema nawashukuru, msinilishe maneno mdomoni,”amesema Lowassa

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha, Loata Sanare amesema kuwa wote waliokwenda upande wa pili wa upinzani wakitaka kurudi lazima wafuate utaratibu kama Lowassa kwani Lowasa licha ya kupokelewa na mwenyekiti wa CCM Taifa aliandika barua kwenye tawi.

Naye Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole amesema kuwa Lowassa amefuata taratibu zote za chama cha mapinduzi hivyo wamejadili na kuona anafaa kurudi CCM bila kuleta mjadala katika chama hicho.

 

Video: Lowassa msiniulize kwanini nimerudi, atoa agizo kwa wapiga kura wake
Rosa Ree kupata mtoto, kukamilisha safari ya kuwa mama