Wakati Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeshapuliza kipenga cha kuanza Kampeni katika ngazi ya urais, ubunge na udiwani kuelekea uchaguzi mkuu, Mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa anaonekana kumtegea mpinzani wake mkuu, Dk. John Magufuli wa CCM.

Hii imebainika baada ya CCM kutangaza rasmi kuwa itazindua kampeni zake Jumapili (Agosti 23) katika viwanja vya Jangwani, Dar es Salaam, Chadema na Ukawa wao wameonekana kutokuwa na haraka ya kuzindua kampeni hizo hasa baada ya taarifa za kukataliwa na Serikali kutumia uwanja mkuu wa Taifa kuwekwa wazi na Idara ya Habari Maelezo hivi karibuni.

Afisa Habari wa Chadema, Tumaini Makene ameliambia gazeti la Nipashe kuwa ngome ya Ukawa haina mpango wa kuzindua kampeni hivi karibuni huku kauli yake ikionesha dhahiri kuwa inawategea CCM kwanza.

“Mgombea wetu hatazindua kampeni leo wala kesho! Waache hao wengine waanze, sisi tunajipanga kupata eneo zuri litakalotosha kwa idadi kubwa ya watu tunaowatarajia ikiwamo na maegesho ya magari,” alisema Makene.

Hali hii haikutarajiwa kwa kuzingatia kuwa muda wa Kampeni ni mfinyu zaidi ya majimbo ya uchaguzi yaliyotengwa.

Hii inaweza kuchukuliwa kama mbinu mojawapo ya kuona wanachofanya wenzao na kuwaonesha zaidi ya hicho hapo baadae.

Taarifa kutoka kwa watu wa karibu wa kambi ya Lowassa zinaeleza kuwa Ukawa wamepanga kuzindua kampeni wiki moja baada ya Magufuli na kwamba wataacha historia.

 

Wasanii Wakubwa Kuwapigia Debe Wagombea Urais, Wanapatia Au Wanapotea?
Diamond Na Wema Sepetu Waanza Kumpigania Magufuli Kwa Vitendo