Vielelezo vinavyoonesha kuwa Kiswahili ni moja kati ya nembo za utambulisho wa Afrika vinaendelea kubainika ambapo mastaa kadhaa wa Marekani wanapotaka kuyakuna masikio ya Afrika Mashariki hutumia lugha hiyo.
Rapa nguli, LL Cool Jay ametumia video ya sekunde 14 kuwashukuru mashabiki wake wa Afrika Mashariki kwa lugha ya Kiswahili.
Rapa huyo ambaye pia ni muigizaji anaonekana kufurahia kile alichokisema kwa kuwa Kiswahili ni kitamu.