Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Rais wa TLS, Tundu Lissu amesema kuwa anasikitishwa na wabobezi wa sheria nchini akiwemo Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe  pamoja na Waziri wa Katiba Na Sheria, Prof. Palamagamba Kabudi kuwa wanashindwa kuishauri vizuri serikali

Lissu amedai kuwa wataalam na wabobezi wa sheria ndani ya serikali wamekuwa hawatekelezi wajibu wao vizuri wa kuishauri serikali kuhusiana masuala ya sheria jambo ambalo linaleta athari kubwa katika nchi, ikiwepo kuzuiwa kwa ndege ya Tanzania aina ya Bombardier Q400-Dash 8

“Nisema hapa kwa masikitiko makubwa kabisaa wanasheria waliobobea ambao wanatakiwa kumuelekeza Rais Dkt. Magufuli sawa sawa wamekuwa hawatekelezi wajibu wao kwa sababu pengine ya kuogopa kutumbuliwa,” alisema Tundu Lissu

Hata hivyo, ameongeza kuwa kabla ya Bunge kumalizika kulijitokeza mjadala kuhusu mikataba aliyohoji uharali wa kuvunjwa kwa baadhi ya mikaba bila kufuata utaratibu, alijibiwa na Dkt. Mwakyembe pamoja na Prof. Kabudi kwamba nchi huru haiwezi kuogopa kushtakiwa katika mahakama ya Kimataifa kwa kuvunja mikatba na kuvunja wajibu wetu kwa Jumuiya ya Kimataifa kwa mujibu wa mikataba ya kimataifa walioisani.

Rais Shein awashukia mawaziri, ‘mnachokitafuta mtakipata’
Ester Bulaya akamatwa na jeshi la polisi