Baraza kuu la Chama cha Wananchi, CUF kupitia Mwenyekiti wake, Profesa Ibrahimu Lipumba imeunga mkono jitihada zinazofanywa na Rais, John Pombe Magufuli na Serikali yake kwa utekelezaji wa mambo katika kujenga nchi.
Lipumba katika mazungumzo aliyoyafanya leo na waandishi wa habari ameiomba Serikali kuangazia swala zima la kodi na kuitaka Mamlaka ya Kodi (TRA), kuacha kuwakamua wafanyabiashara na makampuni kwa kuwatoza kodi kubwa isiyoendana na kipato kinachopatikana kupitia biashara hiyo.
Amesema kwa kufanya hivyo inapelekea biashara nyingi kufungwa kitu ambacho kinailetea nchi hasara kubwa katika nyanja mbalimbali.
“Tunaunga mkono katika ukosaji wa kodi lakini utekelezaji wake uzingatie hali halisi, tusije tukawakamua watu wanaofanya biashara, wenye makampuni ambao wanatoa ajira mpaka biashara na shughuli zao kupelekea kuzifunga”. Amesema Lipumba.
Lakini pia amegusia suala zima la ugumu wa maisha, jambo ambalo linalalamikiwa na watanzania wengi na ameishauri serikali kuongeza mzunguko wa pesa ili kuweza kuinua maisha ya watanzania wa hali ya chini.

TFF yaanza Mchakato wa kumpata Kocha mpya Taifa Stars.
TCRA yaingilia kati mazungumzo ya Diamond dhidi ya Shonza