Mkuu wa wilaya ya Kilwa, Mkoani Lindi, Christopher Ngubiagai amekemea kitendo cha wananchi wilayani humo cha kuwazomea watalii wa kizungu na kuwaita ‘Corona Virus’ na kuahidi kuwachukulia hatua kali wote waliohusika.

Watalii hao walitembelea wilaya hiyo kwaajili ya kuangalia mambo mbalimbali ya kihistoria ambapo walizomewa na kuitwa Corona kitendo ambacho mkuu wa wilaya hiyo amekikemea vikali.

Aidha Ngubiagai ameagiza taasisi binafsi za umma wilayani humo kutengeneza sehemu ya kunawia mikono watu mbalimbali pindi wanapoingia katika ofisi zao ili kuepuka maambukizi ya virusi vya Corona ambapo mpaka hivi Tanzania ina visa 5 vya wagonjwa wa Corona.

Mataifa 180 mpaka sasa yameathirika kutokana na virusi hivyo huku watu 246,972 wakiathirika, watu 10,050 wakipoteza maisha na 88,486 wakipona virusi hiyo.

Video: Kishindo cha Mbowe chamtisha Makonda, Polepole, Maswali magumu vita ya Corona
Mwanamke afungwa minyororo miaka mitatu, abakwa na kuambukizwa HIV

Comments

comments