Msanii wa Bongo Fleva, Linah Sanga amefunguka na kudai hakuwa tayari kuwa na mtoto kipindi hiki ila anamuomba Mungu isiwe kigezo cha yeye kupotea katika muziki ili aje kuwa mfano kwa wasanii wenzake wa kike wanaogopa kubebea ujauzito

Linah amebainisha hayo baada ya kuwepo imani kwa baadhi ya watu wakidai msanii akioa, akiolewa hata akijifungua na mtoto mara nyingi hawezi kuendelea kufanya vizuri katika kazi zake kwa kuwa majukumu ya ulezi yanaongezeka na kupelekea kupotea katika muziki.

“Nina muomba Mungu usiku na mchana nisije kupotea katika muziki kwa sababu ya uzazi, ili iwe mfano hata kwa wengine ambao watakuja nyuma yangu, labda wanaogopa kuzaa kwa kufikiri watapotea. Ila mimi nafikiri ni jinsi mtu mwenyewe anavyoishi na mashabiki zake”, amesema Linah.

Hata hivyo, Linah ameendelea kwa kusema hakuwa amejipanga kupata mtoto katika kipindi hiki ila alikuwa anatamani apate ujauzito japo hakuwa amepanga ni wakati gani ambao utakuwa ni sahihi kwake.

Kwa upande mwingine, Linah amesema anajipa mapumziko katika kufanya kazi zake na kuwataka mashabiki zake wamvumilie mpaka mwakani katika miezi ya mwanzoni ndipo atakapoachia kazi yake mpya.

Azam FC kuja na tuzo zao, timu ya vijana nayo ndani
Hawa ndio mashabiki wa muziki wa Jux

Comments

comments