Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara inatarajiwa kuendelea wikiendi hii kwa michezo nane kuchezwa kwa siku za jumamosi na jumapili katika viwanja nane tofauti nchini ikiwa ni mzunguko wa tatu tangu kuanza kwa ligi hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita.

Jumamosi mabingwa watetezi wa kombe hilo klabu ya Young Africans watakuwa wenyeji wa JKT Ruvu katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, Chama la Wana Stand United watawakaribisha Wana Kimanumanu African Sports katika dimba la Kambarage mjini Shinyanga.

Jijini Mbeya kutakua na mpambano wa wenyeji wa mji huo (Mbeya Derby) kati ya Tanzania Prisons watakapokuwa wakipambana na Mbeya City katika uwanja wa Sokoine jijini humo, huku Maafande wa Mgambo Shooting wakiwakaribisha Wana Lizombe Majimaji FC kwenye uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

Ligi hiyo itaendelea Jumapili kwa michezo minne kuchezaw, Simba SC watawakaribisha Kagera Sugar kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, huku Mwadui FC wakiwa wenyeji wa Azam FC katika uwanja wa Mwadui Complex mjini Shinyanga.

Wakata miwa wa Turiani Mtibwa Sugar watawakaribisha Ndanda FC ya Mtwara kwenye uwanja wa Manungu mkoani Morogoro na Wagosi wa Kaya Coastal Union watakua wenyeji wa Toto Africans katika uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

Eva Carneiro Amuweka Mtegoni Mourinho
Wenger Atetea Maamuzi ya Kumtumia Ospina