Kituo cha Msaada wa Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutoa msamaha kwa wafungwa 8,157 ikiwemo familia ya msanii Nguza Viking.

Pamoja na pongezi hizo LHRC, imesema itaendelea kumuomba Rais Magufuli abadili baadhi ya sheria ikiwemo kuondoa sheria inayotoa ruhusa ya adhabu ya kifo..

“Tunampongeza Rais Magufuli kwa kutoa msamaha kwa wafungwa 61 kati ya wafungwa 522 waliohukumiwa kunyongwa”. LHRC wameandika kupitia ukurasa wao wa Twiiter.

Aidha, Rais Magufuli ametoa msamaha huo kwenye sherehe za maadhimisho ya miaka 56 ya Uhuru wa Tanganyika zilizofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.

 

Hata hivyo, Katika msamaha huo Rais pia amemsamehe mzee Mganga Matonya ambaye ana miaka 85 akiwa amekaa gerezani miaka 37 pamoja na miaka saba aliyokaa mahabusu wakati akisubiri hukumu yake hivyo kufanya afikishe miaka 44 gerezani.

Nchi za Kiarabu zataka kufutwa kwa maamuzi ya Trump
Magazeti ya Tanzania leo Desemba 10, 2017