Uongozi wa Klabu ya Chelsea ya Uingereza umemtangaza rasmi aliyekuwa mchezaji wao wa zamani, Frank Lampard kuwa ndiye kocha mkuu mpya wa kikosi hicho cha The Blues.

Mkataba wa miaka mitatu aliousaini Lampard unatosha kudhihirisha sasa ni kocha mkuu wa kikosi hicho akitokea kwenye timu ya Derby County ambayo alikua akiifundisha hapo awali kabla ya kutua Chelsea timu ambayo aliichezea kwa mafanikio makubwa.

Aidha, Lampard wakati akiwa Chelsea kama mchezaji amefanikiwa kuweka rekodi ya kuwa mfungaji bora wa muda wote katika timu hiyo huku akinyakua mataji kadhaa ikiwemo taji la ligi ya Uingereza mara tatu, FA mara nne, taji la kombe ligi mara mbili, UEFA mara moja na EUROPA mara moja.

Sasa hivi Lampard anachukua nafasi ya kiti cha kocha wa timu hiyo baada ya kuachwa wazi na kocha wa awali aliyekua akikinoa kikosi hicho, Maurizio Sarri kutimkia katika timu ya Juventus ya Italia.

Dkt. Kolimba aviwezesha vikundi vya wanawake mkoani Njombe
LIVE CHATO: Rais Dkt. John Magufuli akimpokea Rais Uhuru Kenyatta