Nyota wa tennis kutoka nchini England, Kyle Edmund amejiondoa kwenye mashindano ya wazi ya Argentina kutokana na kukumbwa na matatizo ya koo.

Edmund anayekamata nafasi ya pili kwa ubora nchini England alikuwa tayari ameingizwa kwenye ratiba ya michuano hiyo, yakiwa ni mashindano yake ya kwanza tangu kumalizika kwa michuano ya wazi ya Australia ambako alifika hatua ya nusu fainali.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 23, anayeshika nafasi ya 26 duniani alikuwa amepangwa kucheza dhidi ya Mhispania Roberto Carballes katika mchezo wa raundi ya kwanza uliokuwa uchezwe leo, Jumatano.

Kwa sasa mchezaji huyo anapatiwa matibabu, na anatarajia kuwa fit baada ya wiki moja huku akitarajiwa kuibukia kwenye mashindano ya wazi ya Rio na endapo atafika fainali ya mashindano hayo atampiku Andy Murray katika nafasi ya kwanza kwenye viwango vya ubora nchini England.

Idd Cheche: Hatujakata tamaa ya ubingwa VPL
JPM afanya uteuzi, apandisha vyeo maafisa wa JWTZ