Mlimbwende Zozibini Tunzi (26) kutoka Afrika kusini amefanikiwa kutwaa taji la Dunia ‘Miss Universe’ katika mashindano yaliyofanyika huko Atlanta, Georgia kwenye studio za muigizaji Tyler Perry.

Hii ni mara ya kwanza kwa mlimbwende mweusi kutoka Afrika kusini kutwaa taji hilo ambapo tayari wamesha wahi kushinda mara mbili, mara ya kwanza ilikuwa mwaka 1978 na ya pili ilikuwa 2017.

Tunzi ambaye ni mwanaharakati na anayependa zaidi kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia ametwaa taji hilo lililokuwa linashikiliwa na Catriona Gray kutoka Ufilipino.

Nafasi ya pili imeshikiliwa na Miss Universe kutoka Puerto Rico, Madison Anderson huku nafasi ya tatu ikishikiliwa na Miss Universe kutoka Mexico, Sofia Arago.

Mbowe, Lipumba uso kwa uso na Magufuli wamuomba Demokrasia
Wanaume Shinyanga waozesha watoto wadogo kwa pombe