Maafisa wa ngazi za juu toka Israel na marekani wamewasili Umoja wa Falme za Kiarabu , kupitia ndege ya kwanza ya kibiashara toka mataifa ya mashariki ya kati ikiwa ni kuweka shinikizo la mahusiano mazuri na ya wazi baina ya mataifa hayo .

Ndege namba LY971 ikiwa imepapwa kwa rangi za bendera ya Israel  iliruka moja kwa moja toka   Tel Aviv na kutua jiji la Abu Dhabi mji mkuu wa Falme za kiarabu  imewasili ikiwa na  Wasaidizi wakuu  wa rais Donald Trump na waziri mkuu wa  Israeli Benjamin Netanyahu.

Pia kwa mara ya kwanza  ndege hiyo ,siku ya jumapili Agosti 30 ilipata kuruka katika anga la nchi ya Saudi Arabia baada ya makubaliano kuanza.

Ndege hiyo iliyobeba viongozi wan chi hizo mbili imechapishwa neno “Amani” kwa lugha ya kingereza, kiibrania pamoja na kiarabu. Pia denge hiyo imepewa jina la Kiryat Gat,ikimaanisha  makazi ya Wayahudi huko  Palestina, Iraq al-Manshiyya na al-Faluja

Agosti 13 ilitangazwa mwanzo wa kuhalalisha ushirikiano wa kimaeneo na makazi  kati ya nchi za kiarabu na Israel ambao kwa kiasi miaka 20 umekuwa ukichochewa hofu toka kwa taifa la Irani

Wapalestina walishutushwa na hatua ya umoja wa Falme za Ki arabu  , hofu ya muda mrefu ingeweza kudhoofisha msimamo wa kiarabu juu ya sakata hili .

Makonda: Waliniita tasa, umenipa mapacha
Wanne bandari mikononi mwa TAKUKURU