Baraza kuu la Umoja wa mataifa liliidhinisha bajeti yake ya dola bilioni 3.07 ambayo kwa mara ya kwanza inajumuisha fedha  kwa  ajili  ya  uchunguzi wa uhalifu wa kivita nchini Syria na Myanmar.

Bajeti  hiyo ina ongezeko  dogo kutoka ile ya  mwaka 2019 ya  dola bilioni 2.9. Ongezeko  hilo  ni  kutokana  na  ujumbe wa  ziada  unaliowekwa  katika  sekretariati  ya  Umoja  wa  mataifa , hali ya maisha kupanda na  marekebisho  ya  kiwango  cha  ubadilishaji fedha.

Kwa  mara  ya  kwanza  bajeti imetengwa kwa  ajili  ya  uchunguzi  nchini  Syria na  Myanmar, ambao hapo awali  ulikuwa  ukigharamiwa  na michango  ya  hiari, lakini mwaka  2020 bajeti ya uchunguzi huo ipo katika bajeti ya  sekretariati  ya  Umoja wa  mataifa  na  itapatiwa  michango  ya lazima  kutoka  kwa  matifa  wanachama  193.

Hata hivyo bajeti  ya  matumizi  ya  Umoja  wa  mataifa  ni  tofauti  kutoka  bajeti ya mwaka  kwa ajili  ya  operesheni  za  kulinda  amani  ya kiasi cha  dola  bilioni 6 ambazo ziliidhinishwa  mwezi  Juni 2019.

Video: Polisi wa kike marufuku kusuka mitindo ya nywele
Man City mambo yazidi kuchacha Uingereza