Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii, Ephraim Kwesigabo amesema kuwa Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia mwezi Februari,2019 umebaki kuwa asilimia 3.0 kama ilivyokuwa mwaka ulioisha  mwezi Januari ,2019.

Ameyasema hayo jijini Dodoma alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa hali hiyo inamaanisha kuwa kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi februari, 2019 imebaki kuwa sawa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi januari 2019.

Amesema kuwa mfumuko wa bei wa mwezi Februari, 2019 kubaki kuwa sawa kama ilivyokuwa mwezi januari, 2019 umechangiwa na kuongezeka na kupungua kwa bei za baadhi ya bidhaa za vyakula na bidhaa zisizo za vyakula kwa kipindi kilichoishia mwezi februari ,2019 zikilinganishwa  na bei  za februari ,2018 .

Katika hatua nyingine kwesigabo amesema kuwa baadhi ya bei za bidhaa zisizo za vyakula ziliongezeka kwa asilimia 2.7,mkaa kwa asilimia 10.1,majokofu kwa asilimia 2.1 na gharama za kumuona daktari hospitali za binafsi ni asilimia 4.6.

Mbali na hilo kwesigabo ameongeza kuwa mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mwezi februari ,2019 umepungunga hadi asilimia 0.5 kutoka asilimia 0.7 ilivyokuwa mwezi januari mwaka ,2019

Hata hivyo, amesema hali ya mfumuko wa Bei kwa nchi za Afrika Mashariki, Uganda mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi februari ,2019 umeongezeka hadi asilimia 3.0 kutoka asilimia 2.7 kwa mwaka ulioishia mwezi januari,2019 huku nchini Kenya mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi februari ,2019 umepungua kidogo asilimia 4.14 kutoka asilimia 4.70 kwa mwaka ulioishia mwezi januari ,2019.

Dkt. Raphael Chegeni awashika mkono Wanawake na Vijana Busega
Mbunge wa Viti Maalumu CCM atoa msaada shule ya msingi Mugeza Mseto