Kufuatia kupatikana kwa mfanyabiashara maarufu nchini, Mohamed Dewji baada ya kutekwa, viongozi mbalimbali wa serikali wamefunguka na kutoa maoni yao.

Katika ukurasa wake wa Twitter, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, January Makamba ameandika kuwa, “Nimemuona na kuongea kwa kirefu Mohamed Dewji, ni mzima wa afya isipokuwa alama za kufungwa kamba mikononi na miguuni, mnamo saa nane usiku watekaji walimtupa katika viwanja vya Gymkana, naamini polisi watatoa taarifa kuhusu kilichojiri, “ameandika Makamba

Kwa upande wake mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe ameandika kwenye ukurasa wake kuwa “Ni jambo la kumshukuru allah, wamemrudisha akiwa salama, mengine tutajadili wakati muafaka ila tunawashukuru wakina Mkumbo kwa nguvu ya allah yatafika mwisho,”ameandika Bashe katika ukurasa wake wa Twitter

Naye aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Dkt. Mwigulu Nchemba kwenye ukurasa wake wa Twitter ameandika kuwa, “Kama si bwana aliyekuwepo pamoja nawe katika kilindi cha waovu, Israeli na aseme sasa, tulikuombea kwa Mungu kwa Imani kubwa sana, ashukuliwe Mungu kwasababu husikia na kujibu machozi yetu, pole kwa yote na hongera sana kwa kurejea salama nhyumbani,”ameandika Mwigulu Nchemba

 

Hii ndiyo sababu ya Mo Dewji kutekwa
Polisi waeleza watekaji walivyoishi na Mo Dewji, ‘walimfunga’