Serikali ya Ghana imeonya kuwa itazifungia ndege za Shirika la Ndege la Uingereza (British Airways) kutua nchini humo baada ya kupata ripoti kuwa kunguni wameonekana katika baadhi ya ndege zake.

Waziri wa Usafiri wa Anga wa Ghana, Cecelia Dapaah ameeleza kuwa endapo shirika hilo halitazingatia hali ya ndege zake Serikali itaweka vikwazo vya kutua nchini humo.

Sakata hilo limetokana na ripoti iliyotolewa na gazeti la Uingereza wiki hii kuwa ndege mojawapo ya Shirika la Ndege la Uingereza iliyokuwa inaelekea Accra ilicheleweshwa kwa zaidi ya saa nne katika uwanja wa ndege wa Heathrow nchini Uingereza baada ya kubainika kuwa kunguni walionekana wakitembea kwenye viti.

Kunguni

Shirika hilo la ndege la Uingereza ambalo ndilo pekee linalofanya safari za Ghana kutoka nchini humo, limetoa taarifa kwa vyombo vya habari likieleza kuwa hali hiyo ilitokea lakini ni kwa kiasi kidogo.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa wataalam wake wamechukua hatua za haraka kuhakikisha wanaondoa tatizo hilo.

Aidha, limeiambia BBC kuwa Ghana inabaki kuwa sehemu muhimu ya ndege zake kutua.

Video: Mtulia arejesha fomu, aahidi kufanya makubwa Kinondoni
Said Ndemla hang'oki Msimbazi