Makazi katika kata ya Kirando mkoani Rukwa pamoja na mabweni mawili ya wasichana katika shule ya sekondari Kirando, yamevamiwa na kunguni ambao wameshindikana kuuawa kwa dawa za kuulia wadudu.

Taarifa za awali kutoka kwa wakazi wa kata hiyo zinaeleza kuwa chanzo kikubwa kinachohisiwa kusambaza wadudu hao ni ongezeko la popo  ambao nao wameshindwa kuwateketeza.

Akithibitisha kutokea kwa janga hilo diwani wa kata ya Kirando, Kakuli Seba amekiri kuwa asilimia kubwa ya nyumba katika kata yake zimevamiwa na kunguni na kusisitiza kuwa ni mlipuko wa aina yake.

Kwa upande wake mkuu wa shule ya sekondari Nkasi ambayo pia imevamiwa na kunguni hao amesema kuwa wanafunzi wake waishio katika mabweni yaliyo na kunguni wanalazimika kukesha usiku katika madarasa yao kwa kuhofia maumivu ya kung’atwa na kunguni.

Aidha amesisitiza kuwa chanzo cha kunguni hao sio uchafu kwakuwa mabweni yanakaguliwa mara mbili kwa wiki, na kueleza kuwa suluhisho la kudumu ni kutengeneza vitanda vya chuma, kwani vilivyopo sasa vya mbao vimegeuka maficho na makazi ya wadudu hao.

“Tumenyunyuzia kila aina ya dawa, nimeshauriwa kutumia mafuta ya ndege lakini baada ya kuelezwa gharama yake nimeshindwa kwani ina gharimu sh. 1,370,000.” ameongeza mwalimu huyo.

Nayo kata jirani ya Itete imeanza kuvamiwa na wadudu hao ambapo Diwani wa kata hiyo Garincha John amedai kuwa hata nyumba yake tayari imesha vamiwa na kunguni pamoja na popo ambao wamegeuka usumbufu kwani hawasikii dawa.

Kwamujibu wa wataalamu wa afya kunguni ni mdudu mdogo wa familia Cimicidae katika oda Hemiptera ya nusungeli Pterygota (wenye mabaya) na anaishi maranyingi katika vitanda na hufyonza damu ya wanadamu kama chakula chake hasa usiku.

 

Lugola awashukia wanaoponda ujio wa ndege mpya
Skendo ya ngono yamtafuna R.Kelly