Kundi la kigaidi la Daesh (ISIS) limetangaza kuwa ndilo lililohusika na milipuko ya mabomu ya hivi karibuni nchini Sri Lanka, milipuko iliyoua mamia ya watu.

ISIS imeyasema hayo kupitia shirika lake la habari za kipropaganda la Amaq, japo bado kundi hilo halijatoa maelezo ya kina wala ushahidi wowote wa kuonesha kuwa ndilo lililohusika na mashambulio hayo.

Hayo yamejiri baada ya vyombo vya usalama nchini humo kuripoti kuwa, mashambulio ya Jumapili iliyopita yalifanywa na magenge ya kigaidi ya nchi hiyo.

Aidha, wapelelezi nchini humo wanasema wanachunguza iwapo waliotekeleza mashambulio hayo ya kigaidi wana uhusiano wowote na mitandao ya kimataifa

Huku hayo yakiarifiwa, idadi ya watu waliopoteza maisha katika mashambulio hidi sasa nchini Sri Lanka imeongezeka na kufikia watu 321.

Msemaji wa polisi nchini Sri Lanka amesema hadi sasa watu 500 wamethibitishwa kujeruhiwa katika mashambulizi hayo ambayo yalilenga makanisa matatu, hoteli nne za kifahari na nyumba.

Video: Mambo ya msingi ziara ya Rais Magufuli nchini Malawi
Wangabo asisitiza kasi ya ujenzi wa hospitali ya wilaya

Comments

comments