Mbunge wa Ubungo kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Said Kubenea amelalamikia suala la Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson kwa kukataa swali la mbunge wa Vunjo, James Mbatia lisijibiwe na waziri mkuu akisema kuwa Naibu Spika amekiuka taratibu za Bunge kwa kupitisha maamuzi ambayo sio sahihi.

Amesema kuwa Dkt. Ackson ametaja sababu alizowahi kuzitoa Spika Ndugai jambo ambalo halina ukweli ndani yake.

“Huu ni mwendelezo wa mamlaka za bunge kuporwa kwa makusudi na uongozi wa bunge kwani kanuni zinasema mbunge yeyote ana haki ya kuhoji kwa waziri yeyote kuhusu mambo ya umma,”amesema Kubenea

Hata hivyo, Jana katika kipindi cha maswali na majibu Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson alikataa swali la James Mbatia lililohoji sababu za serikali kuwatumia barua baraza la maaskofu Tanzania KKKT ikiwataka waufute waraka walioutoa katika kipindi cha kwaresma.

 

Jonny Evans ajiunga na Leicester City
Liverpool walazimisha usajili wa Nabil Fekir