Mkuu wa wilaya ya Korogwe,Kisa Gwakisa ameiagiza kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya kuchunguza watu waliohusika kutaka kuhujumu miundombinu ya reli.

Gwakisa ametoa kauli hiyo baada ya kutokea kwa watu wasiojulikana kutega jiwe kwenye njia ya reli hali ambayo ingeweza kuleta athari kwa treni la abiria linalopita wilayani hapo.

Mkuu huyo wa wilaya amewataka wenyeviti wa vijiji kuunda vikundi vya ulinzi shirikishi kwaajili ya kukagua usalama wa miundombinu hiyo mara kwa mara.

Naye Kiango Singano Mkuu wa reli wilayani hapo ameelezea hali ilivyokuwa huku hii ikiwa ni mara ya pili kwa wilaya ya korogwe kutokea kwa kitendo hicho cha watu kuweka jiwe kwenye barabara ya treni amabapo amomba elimu itolewe zaidi kwa wananchi.

 

Rais wa Congo atishia kuvunja Bunge
Rais Magufuli afanya uteuzi leo