Korea ya Kaskazini imeendelea na mpango wake wa kufanyia majaribio makombola ya masafa marefu hivyo kuendelea kuwa tishio  kwa nchi jirani zake ambao wamekuwa wakipiga kelele kila kukicha kuhusu mipango hiyo.

Kuhusiana na hatua hiyo ya Korea ya Kaskazini kufanya majaribio hayo ya Silaha zenye masafa marefu, Marekani na Korea ya Kusini zimelaani vikali jaribio hilo na kutaka kuongezwa kwa vikwazo kwa Korea ya Kaskazini.

Kwa upande wake Rais mpya wa Korea Kusini Moon Jae-in, amesema kuwa Korea ya Kaskazini imefanya makosa makubwa kufanya majaribio hayo makombora ya masafa marefu huku akisema hatua hiyo ni kitendo cha uchochezi.

Aidha, Moon katika Kampeni zake aliahidi kufanya kazi kwa ushirikiano na utawala wa Korea ya Kaskazini ilikuweza kuangalia namna ya kutaftia ufumbuzi tofauti zilizopo ambazo zimedumu kwa muda mrefu.

Jaribio lingine la Korea Kaskazini liligonga mwamba wiki mbili zilizopita mara  baada ya Umoja wa Mataifa kuweka vikwazo na kufanya majaribio ya zana zake za masafa marefu ya nyuklia.

NEC kulitengea bajeti daftari la wapiga kura
MO aitaka Simba kurudisha fedha zake, adai wamekiuka makubaliano