Korea Kaskazini imetangaza siri ya mpango wake wa kufanya majaribio ya makombora ya masafa marefu na silaha za nyuklia huku ikisema kuwa mpango huo ni kwaajiri ya kuboresha zana za kijeshi na jeshi kwa ujumla.

Katika taarifa iliyotolewa na Shirika la Habari la Korea Kaskazini KCNA imesema kuwa baada ya kombora la mwisho kufanyiwa majaribio, Rais wa nchi hiyo, Kim Jong-Un, amesema kuwa hataki kusikia Marekani ikisema itakabiliana na Korea Kaskazini kijeshi.

Rais Kim amesema kuwa majaribio hayo yote yamefanyika kwaajiri ya kuimarisha jeshi la nchi hiyo ili kulifanya kuwa miongoni mwa majeshi yenye nguvu duniani hivyo kukabiliana na yeyote atakayetishia amani ya nchi hiyo.

“Lazima tuyaonyeshe mataifa yanye uwezo mkubwa wa kijeshi kuwa taifa letu litakavyokamilisha mpango huu wa majaribio ya silaha zetu za masafa marefu na za nyuklia, licha ya vikwazo visivyokuwa na mwisho,”amesema Rais Kim

Hata hivyo, mpango wa Korea Kaskazini wa kufanya majaribio ya makombora ya masafa marefu umesababisha mgawanyiko mkubwa miongoni mwa mataifa ambayo yalikuwa na uhusiano wa karibu na nchi hiyo.

 

Rooney kupokelewa kama mfalme Old Trafford
INAUMA SANA!!: Binti mwenye ugonjwa wa ajabu asimulia mazito, apaza sauti kuokoa maisha yake (+Video)