Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Senegal, Aliou Cisse amesema kuwa licha ya ushindi walioupata jana katika mchezo wao dhidi ya Uganda katika hatua ya 16 bora kwenye michuano ya AFCON lakini amewapongeza wapinzani wao kwa kuonyesha upinzani wa hali ya juu.

Akizungumza baada ya kumalizika kwa mchezo huo, Cisse amesema kuwa Uganda ni timu ngumu kitu ambacho kiliwafanya wacheze kwa kujilinda mara kwa mara licha ya bao la mapema la mshambuliaji Sadio Mane ambalo alifunga katika mtanange huo pia amesema kwasasa nguvu zao wanazielekeza katika hatua ya robo fainali ambayo huenda ikawa ni ngumu zaidi.

”Tumepata ushindi dhidi ya timu ngumu tulipata goli lakini tulizuia kila muda tunatakiwa kujiandaa kwaajili ya hatua inayofuata ambayo ni ngumu zaidi,”alisema Cisse.

Aidha, Mane alifunga bao hilo mnamo dakika ya 14 ya kipindi cha kwanza na kufanikiwa kuivusha timu yake hadi hatua ya robo fainali ambapo mchezo mwingine ulikua baina ya Benin dhidi ya Morocco na timu ya taifa ya Benin ilifanikiwa kuwafunga wapinzani wao kwa mikwaju ya penati.

Video: NDC yatua sabasaba na matrekta kwa milioni 3, yahimiza wakulima kuchangamkia fursa
Video: Wakili Manyama aibua mapya kuhusu Lissu, 'Spika Ndugai hakukosea'