Kocha wa klabu ya soka ya Yong Sports ya Cameroon, Emmanuel Ndoumbe Bosso aliyekuwa ametekwa na watu wasiojulikana, ameachiwa huru.

Kwa mujibu wa BBC, jeshi la polisi la nchi hiyo limeeleza kuwa kocha huyo alitekwa alipokuwa akiendesha gari lake kuelekea zilipo ofisi za klabu hiyo mjini Bameda kwa ajili ya kuendesha mafunzo na mazoezi.

Msemaji wa klabu hiyo, Wanchia Cynthia ameeleza kuwa kocha huyo amejiunga na familia yake na kwamba bado hawajafahamu sababu za kutekwa kwake na kwamba waliomteka hawakuwa na nia ya kujipatia fedha.

“Watekaji hawakudai fedha yoyote kama sharti la kumuachia huru kocha wetu. Tunaamini shinikizo la watu kwenye mitandao ya kijamii kutoka kwa mashabiki pamoja na vyombo vingine vya habari ni moja kati ya jitihada zilizofanikisha kuachiwa kwake,” alisema Wanchia Cynthia.

Aliongeza kuwa hivi sasa chama kimemuacha apumzike na kuviachia vyombo vya usalama kuendelea na kazi yao kuhusu tukio hilo.

Eneo la Bamenda ni moja kati ya maeneo mawili ya watu wanaozungumza kiingereza ambapo kumekuwa na mgogoro na makabiliano kati ya Serikali na kundi la watu wanaopambana na dola kwa miaka mitatu sasa kwa kile wanachodaikuwa kuna ubaguzi dhidi ya wananchi wanaozungumza kiingereza.

Polisi wakamata sanduku la mabilioni ya noti bandia ndani ya benki
Mama aichoma na maji ya moto mikono ya mwanae