Kocha Mkuu wa Simba, Mbelgiji Sven Vandenbroeck amewapongeza wachezaji wake kwa kucheza vizuri na kufanikiwa kulipa kisasi kwa kuibuka na ushindi mkubwa wa mabao manne kwa moja, katika mchezo wa Nusu Fainali Kombe La Shirikisho Tanzania Bara (ASFC).

Kocha Sven amesema mchezo wa Nusu Fainali ulikuwa mzuri kwa wapinzani wake kucheza vizuri kipindi cha kwanza, na walivyopata bao la kwanza alikua na wakati mgumu kuhawahimiza wachezaji wake kujitolea.

Amewataka wachezaji wake kutoridhika na kutwaa ubingwa pamoja na kuifunga Young Africans, na badala yake waelekeza akili na nguvu zao kwenye michezo yao ilizobaki ili kumaliza Ligi Kuu Tanzania Bara kwa heshima kubwa.

Amesema kwa matokeo hayo pamoja na kutangazwa rasmi mabingwa wa Ligi Kuu, haitawafanya kuridhika, bali wanatafuta alama zote tatu katika michezo iliyobaki ili kumaliza kwa heshima kubwa.

“Wamejituma wamecheza kwa kiwango kizuri, lakini bado hatujamaliza ligi, tunahitaji kufanya vizuri na kuheshimu ubingwa wetu kwa kutafuta alama muhimu katika mechi zetu za ligi ikiwamo dhidi ya Mbao FC,” alisema Sven.

“Tunakutana na timu iliyopo chini, ipo katika wakati mgumu itakuja kucheza kwa kukamia kumfunga bingwa, lakini pamoja na kutafuta pointi muhimu zitakazowaweka katika nafasi nzuri kwenye msimamo,” alisema kocha huyo.

Kikosi cha Simba leo kitaingia kambini kwa ajili ya maandalizi ya mechi yao dhidi ya Mbao FC utakaochezwa keshokuwa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Wachezaji Simba SC kukabidhiwa Mamilioni
Ivory Coast: Makamu wa Rais ajiuzulu baada ya kifo cha waziri Mkuu