Mzaliwa wa Ujerumani Cebio Soukou meitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Benin, kwa ajili ya mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Afrika 2019 dhidi ya Gambia, watakaokua nyumbani mjini Banjui Novemba 17.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 26, ambaye wazazi wake wana asili ya Benin, kwa sasa anaitumikia klabu ya Hansa Rostock inayoshiriki ligi daraja la tatu nchini Ujerumani.

Kocha mkuu Michel Dussuyer ametangaza kikosi chake, huku akitarajia kumkosa nahodha na mshambuliaji Stephane Sessegnon, ambaye anatumikia adhabu ya kadi nyekundu.

Mshambuliaji huyo wa klabu ya Gençlerbirliği ya Uturuki, aliadhibiwa wakati wa mchezo wa mkondo wanne wa kundi D dhidi ya Algeria waliokua nyumbani na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa bao moja kwa sifuri.

Naye mchezaji Djiman Koukou amerejeshwa kikosini, baada ya kuonekana kwa mara ya mwisho akiwa amevaa jezi ya timu ya taifa Benin uwanjani, Novemba 2017.

Wachezaji muhimu kama walinda mlango Fabien Farnolle, defender Khaled Adenon, Washambuliaji Mickael Poté na Steve Mounié wote kwa pamoja wametajwa kwenye kiksoi kitakachoikabili Gambia baadae mwezi huu.

Katika mchezo wa kwanza Benin waliifunga Gambia bao moja kwa sifuri mjini Cotonou, mwezi Juni mwaka jana.

Kikosi kilichotajwa kwa ajili ya mchezo wa Novemba 17.

Makipa: Fabien Farnolle (Malatyaspor, Turkey) na Saturnin Allagbé (Niort, France).

Mabeki: Seïdou Barazé (Moulins Yzeure, France), Khaled Adenon (Amiens, France), Moïse Adilehou (Levadiakos, Greece), Chams Deen Chaona (Stade Gabésien, Tunisia), Emmanuel Imorou (Caen, France), David Kiki (Brest, France), Junior Salomon (United Plateau, Nigeria) na Olivier Verdon (Sochaux, France)

Viungo: Jordan Adéoti (Auxerre, France), David Djigla (Niort, France), Jean-Marie Guera (Enyimba, Nigeria), Sessi D’Almeida (Yeovil Town, England), Djiman Koukou (Astra Giurgiu, Romania) na Cebio Soukou (Hansa Rostock, Germany)

Washambuliaji: Jacques Bessan (Tunisian Stadium, Tunisia), Marcellin Koukpo (CS Hammam-Lif, Tunisia), Steve Mounié (Huddersfield, England), Jodel Dossou (FC Vaduz, Liechtenstein), Mickael Poté (Adana Demirspor, Turkey) na Désiré Segbe Azankpo (FK Senica, Slovakia)

Okwi, Pluijm watamba mwezi Oktoba
Fuchs aikacha Ufaransa, Seedorf amuita kuzikabili Morocco, Brazil

Comments

comments