Kocha Salum Shaban Mayanga, huenda akaikacha timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars), na kutimkia nchini Kenya kujiunga na klabu ya AFC Leopards.

Mayanga anatajwa kuwa katika mchakato huo, kufuatia kocha wa sasa wa AFC Leopards Mtanzania Denis Kitambi, kuwa mbioni kuondoka nchini Kenya na kuelekea Bangladesh, kujiungana bosi wake wa zamani Stewart Hall.

Wawili hao walifanya kazi kwa pamoja wakiwa na klabu ya Azam FC ya Tanzania, na sasa wameonekana kutaka kurejesha umoja wao katika ligi ya Bagladesh.

Mayanga ni kocha pekee kutoa Afrika aliye katika orodha ya makocha wanaowania kibarua ndani ya AFC Leopards, huku wengine wakiwa ni Ronalfo Zapata (Argentina), Didier Gomes da Rosa (Ufaransa).

Hata hivyo safari ya Mayanga itategemea na mazungumzo kati yake na uongozi wa shirikisho la soka nchini Tanzania (TFF), ambao umeonyesha nia ya kutaka kumuongezea mkataba wa kuendelea kukinoa kikosi cha Taifa Stars, kufuatia mkataba wake wa sasa kufikia kikomo.

Mayanga amekua na mtiririko mzuri wa matokeo akiwa na timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars), tangu alipoteuliwa na uongozi wa TFF uliopita chini ya Jamal Malinzi.

Mayanga alikabidhiwa kikosi cha Taifa Stars, baada ya kujiuzulu kwa kocha Chrales Boniface Mkwassa Master ambaye kwa sasa ni katibu mkuu wa klabu bingwa Tanzania bara Young Africans.

Uamuzi wa Basata dhidi ya Bill Nas na Nandy
Sergio Aguero kuikosa Tottenham Hotspur