Meneja wa Klabu ya Liverpool, Jurgen Klopp ameweka wazi kuwa hatafuti mbadala wa Philippe  Coutinho katika dirisha hili la usajili.

Liverpool imempoteza mshambuliaji huyo kufuatia kujiunga na Barcelona kwa kitita cha euro million 160.

Aidha, Majogoo hao wa Anfield mpaka sasa wameshamsajili mlinzi, Van Dijk kutoka Southampton huku Klopp akisisitiza kuwa huyo ndo mchezaji pekee aliye sajiliwa na klabu hiyo katika dirisha dogo la usajili.

Hata hivyo, Klop amekaririwa akisema hawezi kuendelea kufikiria kutafuta mbadala wa mshambuliaji badala yake ameelekeza mawazo yake kunye kutumia wacheji alio nao kwa hivi sasa.

 

Yanayojiri Kenya, kuapishwa kwa Odinga
Usain Bolt ajiunga Mamelodi Sundowns