Mkazi wa Manispaa ya Mtwara, Sharifu Issah maarufu kwa jina la Zamda Salum amefikishwa mahakamani kwa kosa la kufanya vitendo kinyume na maadili kwa kujifanya mwanamke na kumshawishi mwanaume mwenzake kufunga ndoa.

Hakimu Mkuu Mkazi, Richard Kabate amesema kuwa kosa hilo ni kinyume na kifungu cha 157 cha kanuni ya adhabu sura namba 16 ya sheria iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

Aidha, Kabate amedai kuwa mshtakiwa kati ya mwezi Machi mwaka huu na mwezi wa Juni akiwa katika vijiji vya Mkahala na Mpanyani halmashauri ya Nanyamba mkoani Mtwara kwa makusudi alijifanya mwanamke na kumshawishi Mustapha Saidi Nurdini kwa kumtongoza na kufunga nae ndoa isiyo halali.

Vile vile ameongeza kuwa kitendo kama hicho kinatoa tafsiri ya ukiukwaji mkubwa wa maadili kwa watu wa jinsia moja ya kiume kuishi kinyumba kama mume na mke.

INAUMA SANA!!: Binti mwenye ugonjwa wa ajabu asimulia mazito, apaza sauti kuokoa maisha yake (+Video)
Morata aeleza sababu za kuitosa Man Utd