Katika hali isiyo ya kawaida, ‘National Environment Management Council’ (NEMC), imebaini kuwepo kiwanda kinachomilikiwa na raia wa Kichina ambacho kinasindika nyama ya Punda.

Hiyo ilibainika jana baada ya Uongozi wa NEMC kutembelea kiwanda hicho na kufanya ukaguzi wa ghafla.

Uongozi wa kiwanda hicho ulikiri kufanya usindikaji wa nyama za punda na kueleza wazi kuwa huchincha zaidi ya punda 200 kila siku huku wakijitetea kuwa nyama hizo haziuzwi nchini bali kupelekwa ughaibuni.

Hata hivyo, baadhi ya wakazi wa Dodoma walieleza kuwa nyama hizo zinasadikika kuwa zinasambazwa sehemu mbalimbali za starehe na kuuzwa kama nyama za ng’ombe.

Mwanasheria wa NEMC, Machali Heche alisema kuwa baada ya kufanya mahojiano ya kina na uongozi wa kiwanda hicho, wameamua kukifunga mara moja kuanzia jana na kwamba punde watawaandikia barua kwa mujibu wa sheria itakayokuwa na faini isiyopungua shilingi milioni 200.

“Nyama ya punda inaweza kusababisha maradhi mengi sana kwa hiyo hii ni hatari sana kwa afya ya binadamu. Kufanya hivi ni ukikukwaji mkubwa wa sheria na haki za binadamu.”

“Watanzania Hawahitaji Mabadiliko, Nilizungumza Nao”
Sakata La Mourinho Na Daktari Wake Lapiga Hatua