Wakulima katika maeneo mbalimbali wamekuwa wakiomba kujengewa viwanda vya kusindika mazo yao kwa muda mrefu, na hatimaye kilio hicho kimesikiwa kwa wawekezaji wa mazao ya jamii ya kunde.

Ambapo kiwanda cha kusindika mazao hayo kimeanza kujengwa mkoani Morogoro ambacho kitawanufaisha wakulima wa mkoa huo pamoja na wale wa mikoa ya jirani.

Ujenzi wa kiwanda hicho kinacho jengwa na na mwekezaji umepongezwa na mkuu wa mkoa wa Morogoro Dk. Stephen Kabwe na kuwataka wakulima wa mazao ya jamii ya kunde kulima kwa wingi kwani watakuwa na soko la uhakika la kuuza mazo yao, kitendo kitakachokuza uchumi wao.

Aidha mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), mkoa wa Morogoro, Inncent kalogeles licha ya kufurahishwa na ujenzi wa kiwanda hicho amesema kuwa ujenzi huo ni moja ya utekelezaji wa ilani katika uchumi wa viwanda na kuwataka wananchi kuchangamkia fursa.

Kwaupande wake mwakilishi wa kiwanda hicho Shaban Tupa amewaeleza viongozi wa mji wa Morogoro kuwa ujenzi utakapokamilika jumla ya watu 1,500 watapata ajira kiwandani hapo nakuwaomba wote watakaopata nafasi kuwa waaminifu.

 

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Januari 13, 2019
Mtumbwi uliotengenezwa na taka za plastiki kuanza safari Kenya - Zanzibar

Comments

comments