Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam, Lazaro Mambosasa amewaonya wafuasi wa Chama Cha Wananchi (CUF) waliojipanga kufanya fujo katika zoezi la kuhesabu kura katika jimbo la Kinondoni.

Ametoa onyo hilo wakati akizungumza na kituo kimoja cha Televisheni jijini Dar es salaam, ambapo amesema vikundi hivyo ni bora vikabaki nyumbani kwani hatasalimika mtu.

Amesema kuwa Jeshi la polisi limejipanga kwa kila kitu kuhakikisha uchaguzi huo wa marudio katika jimbo la Kinondoni unafanyika kwa amani.

“Tumeona kwenye mitandao kuna watu wanakusanyana kutoka Temeke, Ilala na Kinondoni kwa ajili ya kuja kufanya fujo, naomba wabaki nyumbani kwa sababu hakuna atakaesalimika,”amesema Kamanda Mambosasa

Hata hivyo, ameongeza kuwa uchaguzi umefanyika katika hali ya amani na usalama hivyo wananchi wa wa jimbo la Kinondoni hawapaswi kuwa na hofu.

 

Video: Hatushindani na CCM bali tunashindana na Dola- Salum Mwalimu
Sanduku la kupigia kura laibiwa Kinondoni