Kufuatia sheria iliyoundwa Agosti 2015 na Serikali huko Lamu ya kuondoa Magari, Pikipiki, na Baiskeli kwenye mji huo wa kale na kuamuru usafiri wa kutembea kwa miguu na punda pekee, mamlaka ya mji imemuagiza Mkuu wa wilaya Joseph Kanyiri kuwakamata wanaokiuka amri hiyo.

Katika mji huo mkuu na mkongwe uliopo pwani ya Kenya, unawakazi takribani 10,000  na ni mji wa kihistoria ambao ume endelea kuvutia watalii kila kukicha.

Katika sheria hiyo, vyombo vya moto kama pikipiki na magari haruhusiwi kabisa kutumika kusafirisha abiria, na magari pekee yanayofanya kazi ni gari la Polisi, gari la kubebea wagonjwa, gari la mamlaka ya maji, na gari la kuzoa taka mitaani.

Kwa mujibu wa Gavana wa Lamu, Dkt. Issa Timamy nimarufuku kwa mtu yeyote kuingiza chombo cha usafiri nje ya Punda katika kisiwa hicho ambacho kipo umbali wa kilometa 341 kutoka Mombasa.

Raia wengine wote wa kawaida wamekuwa wakitumia miguu miaka nenda rudi, na wale walionakipato kidogo wamekuwa wakitumia Punda na mikokoteni katika safari zao za ndani ya kisiwa hicho cha historia.

Usafiri huo wa Punda unaaminika sana na watu wa kisiwani hapo , kwani licha ya kutumika kubebea watu kwa maana ya abiria au wamiliki wake, wakati mwingine hubeba pia wagonjwa, magunia wenye bidhaa  mbalimbali na hata vifaa vya ujenzi.

Akizungumza na wakazi wa kisiwa hicho, Gavana Timamy amesema kuwa “Lamu ni mji wa kihistoria, magari, baiskeli, na pikipiki vinaharibu ukale wa hapa…polisi wafanye kazi yao kwa kuwakamata wanaokiuka sheria hii” na kususitiza kuwa Magari ya Serilkali yenyewe yataruhusiwa kwa kibali maalumu.

Kutokana na umaarufu na umuhimu wa punda katika kisiwa cha Lamu wamekuwa wanapatikana kwa shida na wamekuwa ghali, wanatunzwa vizuri, huku wamiliki wa wanyama hao wakifanannishwa na watu wanaomiliki magari madogo ya kutembelea au yale yakubebea mizigo.

Wataalamu huamini kwamba mji wa Lamu uliundwa katika karne ya 14, na historia yake ya kwanza iliandikwa kwa rugha ya kiarabu karne ya 16, na kudai kwamba chanzo cha mji huo ni familia moja kutoka Shiraz (Ujerumani), katika karne ya tatu.

Mji ulikuwa na kustawi kwasabau ulitumika kama kituo cha majahazi yaliyotumika kwenye biashara kati ya watu wa pwani ya Afrika mashariki na Bara Arabu pamoja na Uhindi.

Tanzania na Brazil zaingia makubaliano ya kuinua kilimo cha Pamba nchini
Jeshi la Polisi lazuia mkutano wa Prof. Lipumba, 'wakaidi agizo'

Comments

comments